CHAN 2024: Tanzania yavuna alama sita baada ya kuifunga Mauritania

Michuano ya CHAN 2024 inaandaliwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Newstimehub

Newstimehub

6 Agosti, 2025

f8a556a713351fee86b797f0de14979eaf93238d0203f0b8caa0d79c7ec76424

Tanzania imezidi kuchanja mbuga kwenye michuano ya CHAN 2024 baada ya kuifunga Mauritania kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa pili wa Kundi B, uliofanyika Agosti 6, 2025 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Bao pekee la ‘Taifa Stars’ lilifungwa na Shomari Kapombe aka ‘Baba Esther’ katika dakika ya 89 ya mchezo, na kuipa alama nyingine tatu muhimu kwenye michuano hiyo maalumu kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani.

Matokeo hayo yanaifanya Mauritania kubakia na alama moja baada ya suluhu yao ya 0-0 na Madagascar, huku Tanzania ikiongoza kundi hilo, ikiwa na alama sita na magoli matatu, baada ya ushindi wao wa awali dhidi ya Burkina Faso.