CHADEMA: Tumethibitisha Lissu anazuiliwa gereza la Ukonga

Duru kutoka ndanxi ya Chama zinasema kuwa viongozi wawili wa chama hicho pamoja na wanafamilia wachache wameruhusiwa kumuona kupitia kizuizi cha glasi na wamezungumza kwa simu naye.

Newstimehub

Newstimehub

21 Aprili, 2025

2025 01 22t145227z 867001758 rc2p 6 rtrmadp 3 tanzania politics 20 1

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema viongozi wake wamekutana na viongozi wa Jeshi la Magereza na kufahamishwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu amehamishiwa Gereza la Ukonga.

CHADEMA ilikuwa imelitaka Jeshi la Magereza la nchini Tanzania, mamlaka husika na vyombo vya dola nchini humo kutoa taarifa za mahali alipopelekwa Mwenyekiti wao tangu alipokamatwa.

‘‘CHADEMA imewataarifu wananchi kuwa wanaweza kumtembelea kwa kufuata taratibu za kawaida za kumuona mahabusu katika gereza hilo’’ ilisema sehemu ya taarifa katika mitandao ya kijamii.

‘‘Yuko chini ya ulinzi mkali na unaotisha. Ndugu wachache na viongozi Wawili wa Chadema waliruhusiwa kumuona kupitia ukuta mzito wa kioo. Walizungumza naye kwa simu tu,’’ waliendelea kusema.

Ujumbe huo wa CHADEMA ulilalamikia usalama wakielezea kuhofia kuwa huenda anakabiliwa na vitisho na njama za kumdhalilisha.

Hata hivyo CHADEMA imewataarifu wananchi kuwa wanaweza kumtembelea kwa kufuata taratibu za kawaida za kumuona mahabusu katika gereza hilo.

Lissu anazuiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la Uhaini linalomkabili.