Bunge la Uganda lahoji Mamlaka ya Mapato kuhusu gharama ya ukarabati wa magari

Uongozi wa Mamlaka ya Mapato ya Uganda, URA ililieleza bunge kuwa magari yametumika kwa wastani wa miaka 8-12 na kufanyiwa matengenezo makubwa na kati ya magari 6l yaliyochaguliwa, magari 12 yamefanyiwa ukarabati wa injini.

Newstimehub

Newstimehub

15 Septemba, 2025

082641f537b83fee9fb46b0af3048f6f0f929a9069c7d72f6f5d110c34c345a2

Bunge limeibua wasiwasi juu ya gharama za ukarabati wa magari zinazofanywa na Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA) baada ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufichua kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, Mamlaka hiyo ilitumia zaidi ya dola milioni 1.84( UGshs 6.4 bilioni ) kukarabati magari 61, huku kila gari likigharimu wastani wa zaidi ya dola 21,900 ( Ugshs milioni 77).

Gharama kubwa iliyotumika kukarabati gari ikiwa ni zaidi ya dola 30,000 (UGShs106 milioni).

Ufichuzi huo ulitolewa na Medard Sseggona mbunge wa Busiro Mashariki wakati akiwasilisha ripoti ya Kamati ya Tume, Mamlaka za Kisheria na Biashara za Serikali (COSASE) kuhusu ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Mamlaka ya Mapato ya Uganda – Huduma za Biashara ya Disemba 2024, wakati wa kikao cha mawasilisho cha Septemba 11, 2025.

“Gharama hii kubwa katika ukarabati wa magari ni kiashiria cha magari ya zamani yasiyo na thamani kiuchumi,” Sseggona alisema.

Uongozi wa URA ulieleza kuwa magari yametumika kwa wastani wa miaka 8-12 na kufanyiwa matengenezo makubwa na kati ya magari 6l yaliyochaguliwa, magari 12 yamefanyiwa ukarabati wa injini, 21 yalipelekwa mikoani na 16 yalikuwa katika oparesheni za kiuslama