Air Tanzania mbioni kuanza safari za Dar es Salaam-Lagos

Hii ni baada ya shirika hilo kupata kibali cha safari hizo kutoka serikali ya Nigeria.

Newstimehub

Newstimehub

14 Agosti, 2025

e40e7d752f57679c512ed41d0e487e8cd513db161e2c8d2207a7703715ca4ff4

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) liko mbioni kuanza safari za Dar es Salaam hadi Lagos kufuatia kupewa kwa kibali maalumu kutoka serikali ya Nigeria.

Kulingana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya anga ya Nigeria, Ibrahim Abubakar Kana, kibali cha kuiruhusu Air Tanzania kutua nchini humo.

Kibali hicho kitarahisisha ufanisi, kuboresha usalama na kuongeza ushirikiano wa safari za anga kati ya Tanzania na Nigeria.