Watoto 43 kati ya 79 waliouawa katika shambulio la droni ya RSF huko Kordofan Kusini

Mamlaka zinasema kuwa makombora yalipiga shule ya chekechea, hospitali na maeneo ya makazi yenye watu wengi huko Kalogi huku Umoja wa Mataifa ukionya kuhusu kuzorota kwa usalama kote Kordofan.
6 Desemba, 2025
Makubaliano ya Rwanda na DRC yafungua nafasi ya Marekani kuchimba madini

Mnamo Machi 2025, Rais wa DRC Felix Tshisekedi alipendekeza kwa Marekani kuwezesha upatikanaji wa madini ya kimkakati ili kubadilishana na makubaliano rasmi ya usalama.
5 Desemba, 2025
Baadhi ya nchi za Magharibi zataka Tanzania ikabidhi maiti za waliouawa baada ya uchaguzi

Serikali ya Tanzania imetakiwa kukabidhi miili ya waliouawa baada ya uchaguzi mkuu kwa ndugu zao, pamoja na kuwaachia wafungwa wote wa kisiasa.
5 Desemba, 2025
Trump ameipongeza Congo na Rwanda kwa kusaini mkataba wa amani unaosimamiwa na Marekani

Rais Donald Trump aliwapongeza viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda kwa ujasiri wao walipotia saini makubaliano siku ya Alhamisi yenye lengo la kumaliza mzozo wa mashariki mwa Congo na kutoa fursa ya uchimbaji madini kwa Marekani.
5 Desemba, 2025

Marais Paul Kagame, Felix Tshisekedi watia saini mkataba wa kumaliza machafuko mashariki mwa DRC

Marekani ‘kupitia upya’ uhusiano wake na Tanzania

Malawi yaidhinisha matumizi ya sindano ya dawa ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)

Mkuu wa masuala ya haki aonya kuhusu ‘wimbi jipya la ukatili’ katika eneo la Kordofan, Sudan

Afrika Kusini ‘haitashiriki’ G20 chini ya Trump
4 Desemba, 2025
Rais Museveni ataka serikali imiliki mtandao wa intaneti Uganda
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amependekeza kuwa Serikali lazima iwe na mamlaka juu ya mifumo ya msingi ya mtandao ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa bei nafuu.

4 Desemba, 2025
Wabunge Kenya wabaini mwenendo wa utovu wa nidhamu wa wanajeshi wa Uingereza
Mkataba wa sasa wa ushirikiano wa kiulinzi kati ya Uingereza na Kenya ulitiwa saini mwaka wa 2021 na utakamilika mwaka ujao.

3 Desemba, 2025
Tanzania: Gharama za Petroli zaendelea kushuka
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA), bei za mafuta ya petroli na ya taa, zimeendelea kushuka kutokana na kupungua kwa gharama za uagizaji kwa yale yaliyopitia bandari ya Dar es Salaam.

3 Desemba, 2025
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) waahirishwa
Kanuni ya 11 ya uendeshaji wa shughuli za EAC, unataka akidi za nchi zote wanachama zitimie, ili Mkutano wa Wakuu wa EAC ufanyike.

3 Desemba, 2025
Serikali ya Tanzania yamsaka Mange Kimambi
Mange Kimambi amethibitisha kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuwa serikali ya Tanzania imefungua kesi dhidi yake na hivyo kupanga kumrudisha Tanzania.

3 Desemba, 2025
Jeshi la Sudani lachukua tena mji wa Kusini Kordofan baada ya mapambano na vikosi washirika wa RSF
Jeshi la Sudan liliuteka tena mji wa Mabsut katika jimbo la Kordofan Kusini siku ya Jumanne, baada ya mapigano na vikosi vinavyoshirikiana na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), walioshuhudia walisema.

3 Desemba, 2025
Libya inasema kwamba wakimbizi wa Sudan watakuwa kama Walibia na watapata shule, hospitali
Mamlaka ya Libya ilisema Jumanne kwamba itaongeza kasi ya kuwarejesha wahamiaji wa Kiafrika walio chini ya Jangwa la Sahara katika nchi zao, lakini ikasema wakimbizi wa Sudan watachukuliwa kama Walibya na kuruhusiwa kupata shule na hospitali.

2 Desemba, 2025
Papa Leo XIV kutembelea bara la Afrika
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani, analenga kuanza ziara yake hiyo kwa kuitembelea kwanza nchi ya Algeria.

2 Desemba, 2025
Mapigano mapya yazuka siku chache kabla ya Tshisekedi na Kagame kutiliana saini mkataba wa amani
Katika taarifa yake kuhusu mapigano hayo, Jeshi la Ulinzi la nchini DRC (FARDC), limeituhumu Rwanda kwa kushirikiana na kikundi cha waasi wa M23 kwa kuratibu mfululizo wa mashambulizi katika maeneo ya Kaziba, Katogota na Lubarika.

2 Desemba, 2025
Simba Sports Club ya Tanzania ‘yamtimua’ Dimitar Pantev
Pantev alichukua mikoba ya kuwafundisha ‘Wekundu wa Msimbazi’ mwezi Oktoba 2025, akitokea Gaborone United ya Botswana.



