Afisa polisi wa Kenya afariki katika ajali ya barabarani Haiti

Maafisa polisi wanane wa Misheni ya Usaidizi ya Usalama wa Kimataifa (MSS) nchini Haiti wamejeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani Jumapili, huku afisa mmoja wa Kenya akifariki dunia.

Newstimehub

Newstimehub

1 Septemba, 2025

8fdca7f6d2e78bf5c395c1c0faf80d1a162d89618bdd8630fe5f98f666a27aed

Kwa mujibu wa msemaji wa MSS, Jack Ombaka, tukio hilo lilitokea majira ya saa 11 jioni likihusisha magari mawili ya aina ya MaxxPro, ambapo gari moja lilipokuwa likivuta jingine lilipata hitilafu ya kiufundi.

Maafisa waliojeruhiswa pamoja na raia walipelekwa katika Hospitali ya Lambert Santé iliyopo Pétion-Ville, ambapo afisa wa Kenya na raia mmoja walifariki dunia.

“Maafisa wa polisi wanane wa MSS walijeruhiwa, wanne wakiwa katika hali mbaya hivyo wanahitaji kuhamishwa kwa ajili ya kupata matibabu maalum nchini Jamhuri ya Dominika baada ya kupokea huduma ya kwaza katika Hospitali ya Aspen Level 2,” alisema Ombaka katika taarifa yake.

Aidha, Ombaka alitoa rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha baada ya tukio hilo.