“Mimi ni mcha Mungu”: Trump asema ataenda mbinguni baada ya kufariki

Rais wa Marekani alisema huenda asiweze kuwasamehe baadhi ya maadui wake wa kisasa.

Newstimehub

Newstimehub

9 Novemba, 2026

e3fa2667 b674 43e8 ad6e 47115e304d25 1794252312390

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema anaamini ataenda mbinguni baada ya kufariki dunia, akieleza kuwa yeye ni mcha Mungu, licha ya kukiri kuwa huenda asiweze kuwasamehe baadhi ya maadui zake wa kisiasa.

Kauli hiyo aliitoa katika mahojiano na kipindi cha 60 Minutes, alipoulizwa, iwapo kunusurika katika majaribio kadhaa ya mauaji kumebadilisha mtazamo wake kuhusu kifo na mwisho wa maisha yake.

Aliulizwa pia: “Unafikiri nini hutokea mtu anapokufa?”

Trump alinyamaza kwa muda kabla ya kujibu: “Naam, ninatumaini nitakumbukwa.”

Alipoendelea kujibu, alisema: “Mimi ni mcha Mungu, kwa hiyo, kinadharia, ninaenda mbinguni. Natumaini hivyo. Sitaki kwenda motoni.”

Hata hivyo, mazungumzo yalichukua mwelekeo mwingine baada ya kuulizwa iwapo angeweza kuwasamehe wapinzani wake wa kisiasa ili aweze kuingia peponi.

Akijibu swali hilo, Trump alisema wazi kuwa hawezi kufanya hivyo.

“Jibu ni hapana. Nataka kuwa mkweli, hapana,” alisema.

Aliongeza: “Huenda nisiweze kufanya hivyo, hapana, kwa sababu ninawachukia baadhi ya maadui zangu na nitawachukia daima.”