Wahamiaji 20 wapoteza maisha wakijaribu kuvuka maji kuelekea Ugiriki

Kwa mujibu wa mamlaka za Ugiriki, miili 12 ilipatikana ikiwa ndani ya boti moja na mengine 12 ikipatikana kwenye nyingine, huku abiria wengine 40 wakiokolewa katika pwani ya nchi hiyo.

Newstimehub

Newstimehub

9 Novemba, 2026

141dd42a 16af 4208 b111 ac8f3bf26182 1794217715079

Watu 20 wamepoteza maisha baada ya boti waliyokuwa wakiitumia kukumbwa na dhoruba na kuzama kusini mwa kisiwa cha Crete, kilichopo Ugiriki.

Kwa mujibu wa mamlaka za Ugiriki, miili 12 ilipatikana ikiwa ndani ya boti moja na mengine 12 ikipatikana kwenye nyingine, huku abiria wengine 40 wakiokolewa katika pwani ya nchi hiyo.

Mamlaka za Ugiriki zimefanikiwa kuwaokoa manusura 28 na kuopoa mwili mmoja, wote wakiwa ni raia wa Sudan.

Katika tukio lingine, miili 12 ilipatikana katika boti moja kusini mwa kisiwa cha Crete huku manusura wengine 18 wakiokolewa katika kisiwa cha Crete, wakati wahamiaji hao wakijaribu kuingia Ulaya, kupitia Libya.