Rais Hakainde Hichilema wa Zambia anaendelea kuongoza matokeo ya awali ya uchaguzi nchini humo.
Kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ZEC), Hichilema anaongoza kwa asilimia 59 ya kura zote, huku mpinzani wake, Brian Mundubile kutoka chama cha NRPUP akishika nafasi ya tatu.
Hata hivyo, ushindi wa Hichilema umepokelewa tofauti na waangalizi wa kimataifa, wakisema haukuwa wa haki.
Ijumaa iliyopita, mchakato wa kuhesabu kura ulisitishwa kwa saa sita, baada ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kudaiwa kushambuliwa.
Hata hivyo, ZEC imesema hali hiyo imedhibitiwa kwa sasa.
Mmoja ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura jijini Lusaka, aliuawa siku ufunguzi wa upigaji kura, huku watuhimiwa tisa wakikamatwa kufuatia tukio hilo.















