Kipindupindu chaua 170 nchini Sudan

Katika taarifa yake ya Jumatatu, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA), imesema kuwa inaendelea kuratibu shughuli za misaada katika maeneo yaliyoathirika zaidi nchini humo.

Newstimehub

Newstimehub

28 Julai, 2026

d15beb4a c464 4912 ac8a bf915db555fe 1785229065508

Ugonjwa wa kipindupindu unaendelea kusambaa nchini Sudan, ambako watu zaidi ya 2,000 wanahofiwa kuambukizwa na wengine 170 wakipoteza maisha katika eneo la Kordofan.

Katika taarifa yake ya Jumatatu, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA), ilisema kuwa inaendelea kuratibu shughuli za misaada katika maeneo yaliyoathirika zaidi nchini humo.

“Kipindupindu kinazidi kusambaa nchini Sudan, hususan katika eneo la Kordofan,” lilisema shirika hilo.

Licha ya misaada inayoendelea kutoa, shirika hilo limeonya kuwa uhaba wa fedha unaendelea kutia dosari shughuli za za misaada.

Julai mwaka huu, Shirika la Afya Duniani (WHO), lilitadhaharisha kuwa, ugonjwa huo ulikuwa unazidi kuenea katika maeneo ya Darfur na Kordofan, baada ya kutokea vifo 114 na zaidi ya maambukizi 1,330 kuripotiwa.