Baraza jipya la mawaziri lina wanawake tisa, pamoja na watu ambao walikuwa sehemu ya serikali huku wengine wakiingia kwa mara ya kwanza.
Rais wa Madagascar Michael Randrianirina amechangua baraza jipya la mawaziri 30 Jumatano, akibadilisha serikali iliyopita pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu Herintsalama Rajaonarivelo.
Baraza hilo jipya la mawaziri lilitangazwa katika ikulu ya Lavoloha, iliyopo kusini mwa mji mkuu wa Antananarivo, likijumuisha mawaziri 17 ambao walikuwa sehemu ya serikali na 13 wapya.
Kati yao, ni wanawake tisa, pamoja na Mamitiana Rajaonarison, aliyekuwa mkuu wa kupambana na rushwa ambae aliteuliwa kuwa waziri mkuu mwanzoni mwa mwenzi huu.
Chanzo: Newstimetr














