Rais Samia aomboleza kifo cha William Lukuvi

Asema taifa limepoteza mtumishi mwadilifu na mzalendo.

Newstimehub

Newstimehub

25 Mechi, 2026

5689

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kwa huzuni kifo cha aliyekuwa Waziri na Mbunge wa Isimani, William Lukuvi, kilichotokea Machi 25, 2026 katika hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais amesema taifa limepoteza kiongozi shupavu na mwadilifu aliyelitumikia taifa kwa uaminifu mkubwa. Ameongeza kuwa juhudi na mchango wake katika maendeleo ya nchi utaendelea kuenziwa daima.

CHANZO: Newstimetr