Serikali ya Rwanda imeendelea kutekeleza mpango wa kuwarejesha wakimbizi wa Burundi waliokuwa wakiishi nchini humo.
Katika zoezi la hivi karibuni, wakimbizi 74 walivuka mpaka wa Nemba ulioko wilaya ya Busegera wakielekea nchini Burundi.
Afisa wa wizara ya dharura ya Rwanda, Gonzague Karagire, amesema wakimbizi hao walijisajili kwa hiari kabla ya kuruhusiwa kurejea nchini mwao.
Ameongeza kuwa serikali ya Rwanda inafanya kazi kwa karibu na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi kuhakikisha usalama wa wakimbizi hao wakati wa safari na baada ya kufika nyumbani.
CHANZO: Newstimetr














