Jeshi la Congo na waasi wa AFC-M23 watupiana lawama kwa kuvunja makubaliano ya usitishaji mapigano yaliyopendekezwa na Angola.
Mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kundi la waasi la AFC-M23 yameanza tena mashariki mwa nchi, licha ya pendekezo la kusitisha vita lililotolewa wiki iliyopita na Rais wa Angola, João Lourenço.
Pande zote mbili zinatuhumiana kwa kukiuka makubaliano hayo. Serikali ya Kinshasa inadai waasi wanatumia mazungumzo ya kidiplomasia kama kisingizio cha kuimarisha nafasi zao kijeshi katika maeneo wanayodhibiti.
Chanzo: Africanews














