Iran yamnyonga ‘shushushu’ wa Israel

Kulingana na shirika la habari la Fars, mtu huyo anatuhumiwa kutoa taarifa za siri kwa shirika la ujasusi la Mossad la nchini Israel.

Newstimehub

Newstimehub

28 Januari, 2026

b9fe5069c9c27b192b09b29ddd7205173d46250b0cd8c6a453c3eeb4abc0b6f6

Iran imemuua kwa kumnyonga mtu mmoja anayesadikiwa kufanya ushushushu kwa niaba ya Israel, baada ya Mahakama Kuu ya nchi hiyo kuidhinisha hukumu hiyo.

Mtu huyo, aliyetambulika kama Hamidreza Sabet Esmailpour, alikamatwa mwezi Mei 2025, na majeshi ya Iran.

Mamlaka za Iran, zinamtuhumu mtu huyo kwa kutoa taarifa za siri, akishirikiana na Mossad.

Kulingana na wapelelezi wa nchini Iran, mtu huyo anadaiwa kutuma nyaraka nyeti kwa afisa intelijensia wa Israel.

Mamlaka za Iran, pia zinamtuhumu mtu huyo kwa kufanya ushushushu kwa niaba ya Israel, ikiwemo ununuzi wa vifaa vya kiitelijensia na magari kwa ajili ya kufanya hujuma dhidi ya mitambo ya makombora yaliyo chini Wizara ya Ulinzi ya Iran.

Mamlaka za Iran zimezima huduma za intaneti nchini humo, kufuatia mfululizo wa maandamano dhidi ya serikali, yaliyoanza mwezi uliopita.