Mhifadhi wa Tembo Afrika Mashariki Iain Douglas-Hamilton afariki dunia

Mhifadhi huyo alizaliwa na kukulia nchini Uingereza, ingawa muda mwingi wa kazi zake, alitumia akiwa Uganda, Tanzania na Kenya ambako ndipo yalipokuwa makazi yake hadi umauti ulipomkuta.

Newstimehub

Newstimehub

9 Desemba, 2025

57f636508f4f6be7f54debfc21a9a289c950640b4fc8b3b684d9912c364a4dbf scaled

Mhifadhi wa wanyamapori na mazingira kutoka Scotland Iain Douglas-Hamilton, amefariki dunia.

Douglas Hamilton, ambaye alijipatia umaarufu kwa uhifadhi wa Tembo katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda amefariki dunia Disemba 8, 2025 jijini Nairobi, akiwa na umri wa miaka 83.

Mhifadhi huyo atakumbukwa kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa mapambano dhidi ya ujangili wa tembo katika eneo la Afrika Mashariki.

Kazi hiyo ilipelekea kupigwa marufuku kwa biashara haramu ya pembe za ndovu.

“Kazi yake iliweka misingi ya tafiti mbalimbali kuhusu wanyamapori, hasa tembo,” ilisema taasisi ya Save the Elephant kupitia taarifa yake.

Mhifadhi huyo alizaliwa na kukulia nchini Uingereza, ingawa muda mwingi wa kazi zake, alitumia akiwa Uganda, Tanzania na Kenya ambako ndipo yalipokuwa makazi yake hadi umauti ulipomkuta.