Ripoti: Ofisi ya Rais Ruto yatumia zaidi ya dola elfu 15 kwa huduma za uchapishaji kwa siku

Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kenya imetumia zaidi ya dola elfu 15 sawa na shilingi milioni 2 za Kenya kwa siku katika huduma za uchapishaji katika mwaka uliopita wa kifedha.

Newstimehub

Newstimehub

3 Septemba, 2025

1756892206432 lw77xq 6091755908ceec6e7c6fa7f6c1d6f6de89c2ae7497bc7502770a1ab832bd6e7b

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msimamizi wa Bajeti, Bi Margaret Nyakang’o.

Ripoti hiyo, ambayo imebainisha matumizi ya kupindukia na yasiyo ya lazima serikalini, imeonyesha pia kuwa ofisi ya Rais William Ruto ilitumia zaidi ya dola milioni 7 sawa na shilingi bilioni 1 za Kenya kwa ajili ya malipo ya washauri wake, ambao sasa wamefikia 20 chini ya utawala wa Kenya Kwanza.

Licha ya ahadi zilizotolewa za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ili kuziba pengo la bajeti, ripoti inaonyesha kuwa serikali haina utashi huo.