Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amewaachisha kazi mawaziri wake watatu, akiwemo na gavana wa jimbo la magharibi la Bahr el Ghazal, katika mabadiliko aliyoyafanya kwenye baraza lake la mawaziri siku ya Jumatatu.
Kupitia tamko take lililorushwa na Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC), Salva Kiir amemfuta kazi Waziri wake wa Sheria Wek Mamer Kuol na kumteua Joseph Geng Akec kama mbadala wake.
Katika hatua hiyo hiyo, Kiir amemteua Mary Nawai kama Waziri wa Vijana na Michezo, akichukua nafasi ya Akec.