Jeshi la Sudan lakanusha kushambulia kwa bomu msafara wa msaada wa WFP Darfur

Jeshi la Sudan limekanusha madai ya wapiganaji wa RSF kuwa limefanya mashambulizi ya angani dhidi ya msafara wa misaada wa shirika la Mpango wa Chakula (WFP) uliokuwa unapeleka misaada Darfur.

Newstimehub

Newstimehub

21 Agosti, 2025

9ed1b057c7420e7a4b1eff632749f379921dbb8c05844300c97ba9814b516c67

Jeshi la Sudan limekanusha madai ya wapiganaji wa RSF kuwa limefanya mashambulizi ya angani kwa msafara wa misaada wa shirika la WFP lililokuwa likipeleka misaada Darfur.

Katika taarifa iliyosambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, jeshi limesema kuwa madai ya RSF yalikuwa ya “uongo” na yenye lengo la kuficha kile walichokieleza kuwa ni mashambulizi ya wapiganaji dhidi ya msafara katika mji wa Mellit.

Taarifa hiyo imeshtumu RSF kwa kuendeleza “ukiukaji” tangu kuanza kwa mapigano. Pia ilidai kuwa wapiganaji wamefanya kambi za wakimbizi wa ndani kama maeneo ya mafunzo wakisaidiwa na mamluki.

“Serikali, ambayo ilifunguwa njia ya misaada, ikiwemo mpaka wa Adré wa Sudan na Chad, haiwezi katika mazingira yoyote kulenga msafara unaobeba misaada kuwapelekea watu wetu,” jeshi limesema.