Uturuki inaendeleza juhudi za kidiplomasia zenye lengo la kumaliza mapigano nchini Libya na kuwa na “Libya yenye umoja”, kulingana na vyanzo vya wizara ya Ulinzi ya Uturuki
Msukumo huo umeanza kwa ziara ya Mkuu wa Majeshi ya Nchi Kavu wa Libya, Luteni Jenerali Saddam Haftar, Uturuki Aprili 2025.
Mapema wiki hii, meli ya jeshi la wanamaji ya Uturuki TCG Kınalıada ilifanya ziara katika bandari ya Tripoli ambapo kulikuwa na mkutano kati ya Balozi wa Uturuki nchini Libya, Güven Begeç, na waziri wa ulinzi wa Libya, mkuu wa majeshi, kamanda wa jeshi la wanamaji, kamanda wa ulinzi wa maeneo ya bahari na kamanda wa Tripoli.
TCG Kınalıada inatarajiwa kufanya ziara bandari ya Benghazi siku ya Jumatano, wakati ambapo kutakuwa na ziara ya kijeshi na makaribisho rasmi kwenye meli hiyo.
Mtazamo wa kuleta uthabiti