Jamhuri ya Afrika ya Kati itafanya uchaguzi wake mkuu Disemba 28, baada ya kuahirishwa mara kadhaa, afisa wa serikali alithibitisha siku ya Jumanne.
Wapiga kura watashiriki katika uchaguzi wa urais, ubunge, serikali za mitaa na manispaa, Bruno Yapande, waziri aliwaambia waandishi wa habari, kufuatia mkutano na tume ya uchaguzi, ambayo na jukumu la kuweka sawa daftari la wapiga kura.
Mchakato wa uchaguzi unaendelea vizuri, licha ya kuwepo na changamoto, alisema.