Marekani yaweka sheria kali za viza kwa raia wa Nigeria, yachunguza mitandao ya kijamii ya waombaji

Hii ni sheria ya hivi karibuni ya Marekani huku uongozi wa Trump ukiendeleza ukali dhidi ya wahamiaji, hasa wakilenga nchi za Afrika.

Newstimehub

Newstimehub

18 Agosti, 2025

410b9ffcfe6fe975230406e76c358c6b28f58f9e3b8d261be5e70b41d1c24e8d

Marekani imetangaza masharti mapya ya viza kwa raia wa Nigeria, yanayohitaji waombaji wote kuweka wazi akaunti zao za mitandao ya kijamii katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa lengo la kufanyiwa mchujo.

‘‘Kutoweka taarifa za mitandao ya kijamii kunaweza kusababisha mtu kunyimwa viza na uwezekano wa kukosa viza katika siku za baadaye,’’ Ubalozi wa Marekani nchini Nigeria ulisema katika taarifa kwenye mtandao wa X siku ya Jumatatu, ukiongeza kuwa wanaotuma maombi ya viza ‘‘wanahitaji kuweka wazi akaunti zao za mitandao yote ya kijamii ambayo wametumia katika kipindi cha miaka 5 iliyopita katika fomu ya maombi ya DS-160.’’

Serikali ya Nigeria bado haijasema lolote kuhusu taarifa hii mpya ya viza za Marekani.