Israel yapeleka msaada Sudan Kusini huku ikiendeleza njaa Gaza

Hatua hii inakuja huku kukiwa na taarifa za Sudan Kusini kuwa katika mpango wa kuwapa makazi Wapalestina.

Newstimehub

Newstimehub

18 Agosti, 2025

bad8f2e63ace96fba18a663ce86d7e1b90bbbe89a666d9469fdc3f533b7c01ff

Siku ya Jumatatu Israel ilisema itatuma msaada Sudan Kusini, huku Israel ikiendelea kuwa pingamizi kwa Ukanda wa Gaza ambapo imeacha watu wakiwa katika baa la njaa.
Katika taarifa iliyotolewa na Redio ya Jeshi, Wizara ya Mambo ya Nje inasema Israel itatoa msaada wa dharura kwa Sudan Kusini kufuatia mlipuko wa kipindupindu ambao umeenea tangu Septemba 2024.

Chombo cha habari cha umma cha Israel KAN kinasema tangazo hilo linakuja “huku kukiwa na ripoti za majadiliano na Sudan Kusini kuhusu kuwapeleka wakazi wa Gaza kwenye eneo hilo,” Ingawa serikali ya Sudan Kusini ilikanusha kuwepo kwa makubaliano hayo.

Kulingana na gazeti hilo Israel Hayom, msaada huo, unaosimamiwa na Waziri wa Mambo ya Nje Gideon Saar, utajumuisha dawa, vifaa vya kusafisha maji, na vyakula.
Tangazo hilo limeshtua watu kwa sababu Israel imefunga mpaka wa kuingia Gaza tangu Machi 2, ikizuia kupita kwa msafara wa misaada na kuruhusu tu kiasi kidogo ambacho hakitoshi kusaidia watu.

Mashirika ya haki za binaadamu na maafisa wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakishtumu Israel kwa kutumia njaa kama silaha katika vita dhidi ya watu wa Gaza.
Mwezi uliopita, Saar alikuwa mwenyeji wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini Mundi Samaia Kumba mjini Jerusalem, akimshkuru kwa namna nchi yake inavyounga mkono Israel. Wakati wa ziara hiyo, Kumba alitembelea makazi ya walowezi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.