Wanaoshukiwa kuwa waandamanaji wachoma jengo la serikali Afrika Kusini

Waziri wa Mambo ya Ndani Leon Schreiber anasema idara inakusanya ushahidi na itaandaa mashtaka ya jinai dhidi ya wale waliohusika

Newstimehub

Newstimehub

12 Agosti, 2025

25cdddb3b8f70aa94b1de738b6598b803ad37b56e4449a5c864d2a9c52bd96a0

Siku ya Jumanne waandamanaji wanadaiwa kuchoma moto jengo la ghorofa mbili la Wizara ya Mambo ya Ndani huko Germiston, katika mji wa Ekurhuleni karibu na Johannesburg, wakati wakipinga kuondolewa katika nyumba zao.

Waandamanaji walifunga barabara Germiston Jumanne asubuhi kupinga kuondolewa katika nyumba zinazomilikiwa na manispaa, ambapo inadaiwa wamekuwa wakiishi bila kulipa kodi.

“Tulipigiwa simu saa moja asubuhi za hapa na kugundua kuwa sehemu ya paa kwenye ghorofa ya kwanza la Wizara ya Mambo ya Nje limeporomoka,” William Ntladi, Msemaji wa usimamizi wa majanga na dharura wa Ekurhuleni, aliwaambia waandishi katika eneo la tukio.

Alisema chanzo halisi cha moto huo bado hakijajulikana kufikia sasa. Hata hivyo, aliongeza kuwa itakuwa ni wahalifu, huku wengine wakidaiwa kutumia bomu la petroli kuchoma jengo hilo.