Misri inasema haitoacha haki ya maji yake huku kukiwa na mvutano kuhusu bwawa la Nile na Ethiopia

Rais wa Misri anasema suala la maji ya Nile ni madai ya sehemu ya shinikizo kuhusu malengo yasiyohusiana na suala hilo

Newstimehub

Newstimehub

12 Agosti, 2025

c582831e971a146d98f24b4e40bfd512efb6fa6f3262b07e1a6e2fbf8a69ba32

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amekataa hatua ya upande mmoja kuhusu Mto Nile, akionya kuwa yeyote anayeamini kuwa Misri itatelekeza haki za maji yake “amekosea.”

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni, Sisi anasema maji wanayopata kwa mwaka kutoka kwenye vyanzo vyote vya mito ya Nile ni kiwango cha bilioni 1,600, ambayo mengi yanapotea katika misitu, maeneo oevu, na kwenye ardhi.

“Ni kiwango kidogo ambacho kinafika Nile, na hiyo ni Misri na Sudan kwa pamoja wanapata bilioni 85 – ikiwa ni asilimia 4 ya idadi yote,” aliongeza.

Kiongozi huyo wa Misri alisisitiza kuwa kuiachia sehemu yao ya maji “kutamaanisha kuachia maisha ya Misri kabisa,” huku nchi ikikosa njia mbadala ya maji na kuwa na kiwango kidogo cha mvua.