Jeshi la Nigeria laua zaidi ya ‘wapiganaji’ 100 katika mashambulizi ya angani,ardhini

Kulingana na taarifa, mashambulizi hayo ya kijeshi yanaweza kuwa ni kujibu uvamizi wa wapiganaji wa mara kwa mara, hasa utekaji mwezi uliopita.

Newstimehub

Newstimehub

11 Agosti, 2025

c64291db22760ab2033bdc3129e88f883e0ecff9fb4172320a62655abd00c75b

Jeshi la Nigeria limewaua wapiganaji zaidi ya 100 wa genge la wahalifu katika mashambulizi ya angani na ardhini mwishoni mwa wiki, kulingana na taarifa za Umoja wa Mataifa zilizoonekana na shirika la AFP Jumatatu.

Makundi haya ya wapiganaji yamekuwa yakishambulia wakazi kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria,kuvamia vijiji, kuteka wakazi kwa kutaka kulipwa kikombozi na kuchoma nyumba baada ya kupora.

Mashambulizi haya ya kijeshi katika eneo lenye mapigano jimbo la kaskazini magharibi la Zamfara yalifanyika usiku wa manane Jumapili katika eneo la Bukkuyum, ambapo ndege za kivita kwa ushirikiano na vikosi vya ardhini ziliwashambulia wapiganaji zaidi ya 400 waliokuwa wamekusanyika katika kambi ya msitu wa Makakkari.

Mashambulizi haya ya kijeshi “huenda ikawa ni majibu ya uvamizi wa mara kwa mara wa wapiganaji, hasa utekaji nyara, katika jimbo hilo mwezi uliopita,” taarifa hiyo inasema, ikionesha uhusiano na kupungua kwa harakati za kijeshi hivi karibuni katika jimbo hilo na mashambulizi kadhaa ya wapiganaji.

Siku ya Ijumaa kijiji cha Bukkuyum Adabka kulikuwa na mashambulizi ya wapiganaji na watu kadhaa walitekwa na maafisa wa usalama 13 kuuawa.

Vurugu kuenea