Hati fungani kwa ajili ya ujenzi wa uwanja Kenya

Ujenzi wa uwanja wa Talanta unatarajiwa kuimarika baada ya hafla ya kupiga kengele rasmi na Rais William Ruto katika Soko la Hisa la Nairobi.

Newstimehub

Newstimehub

26 Julai, 2025

890c6363bcf75635a11bb7fa12492f66997ce0d2068b97e973ad828f5152449e

Hili limefanyika wakati wa kuwekeza hati fungani za kampuni ya Linzi 003 kwa ajili ya miundombinu.

Uwekezaji huu wa kwanza wa aina yake nchini Kenya, umesaidia kukusanya karibu dola milioni 350, ambazo zitaelekezwa moja kwa moja katika ujenzi wa uwanja wenye uwezo wa kuingia watu 60,000 wa Talanta.

Hati fungani hii ni mfumo wa fedha ambapo wawekezaji wanatoa pesa alafu wanafaidika kwa kupata riba na mkopo huo unakuwa na bima kwa ajili ya miradi maalum ya miundombinu.

Rais Ruto, akizungumza wakati wa hafla hiyo, alieleza uwekezaji huo kama “mfano mzuri wa namna soko la fedha linaweza kuongoza katika mabadiliko ya nchi.”

Ruto alipongeza Soko la Hisa la Nairobi (NSE), Kampuni ya Linzi FinCo Trust, na washirika wake wa LIAISON kwa juhudi zao za kuunganisha sekta binafsi na za umma.