Erdogan aisindikiza meli ya kuzalisha gesi ya Uturuki Bahari Nyeusi

Kadiri Uturuki inavyoendelea kuwekeza kwenye uzalishaji wa gesi ya ndani, ndivyo Osman Gazi inavyozidi kuongeza nafasi ya nchi kujitegemea katika usalama wa nishati na ulinzi.

Newstimehub

Newstimehub

29 Mei, 2025

924ff8ec7b1f97f6bc104981a0fd28af59c2c3b215bbbbce8856680813fb422a

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekisindikiza chombo cha Osman Gazis kinapoelekea katika eneo la Sakarya lililopo Bahari Nyeusi.

Chombo hicho kinatarajiwa kuongeza uzalishaji wa gesi asilia kutoka eneo hilo.

Tukio hilo limefanyika jijini Istanbul, huku Waziri wa Mali Asili Alparslan Bayraktar Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun wakihudhuria.

Bendi maalumu, iliyokuwa ikitumia mahadhi ya kiOttoman, ilitumbuiza wakati wa shughuli hiyo.

Siku hiyo, ambayo pia iliadhimisha kukombolewa kwa Istanbul, Osman Gazi ilianza safari yake kupitia lango kuu la Istanbul, safari inayotegemea kuchukua saa 11.

Chombo hicho kinatarajiwa kuwasili katika bandari ya Filyos Juni 1.

Rais wa Erdogan alipata fursa ya kuzungumza na nahodha wa chombo hicho, na pia alikipanda ili aweze kujionea hali halisi.

“Safari njema,” alisema Erdogan. “Tunatarajia kupata gesi nyingi kutoka Sakarya.”