Kenya inaunga mkono mpango wa mamlaka ya kujisimamia Sahara Magharibi chini ya ufalme wa Morocco

Kenya, baada ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi mbili na Morocco, pia ilifungua ubalozi huko Rabat siku ya Jumatatu.

Newstimehub

Newstimehub

27 Mei, 2025

2025 05 26t231638z 1 lynxnpel4p0rc rtroptp 3 morocco kenya westernsahara

Kenya ilisema Jumatatu inaunga mkono mpango wa Morocco wa kulipa eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi uhuru wa kujisimamia chini ya mamlaka ya ufalme huo wa Afrika Kaskazini, ikiungana na idadi inayoongezeka ya nchi za Kiafrika, Kiarabu na Magharibi ambazo zimeelekea kuunga mkono Rabat katika mzozo wa miongo mitano.

Mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu tangu mwaka 1975, unaikutanisha Morocco, ambayo inachukulia eneo hilo kama himaya yake, dhidi ya mrengo wa Polisario unaoungwa mkono na Algeria, ambao unatafuta taifa huru kabisa katika eneo la jangwa.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mazungumzo kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili mjini Rabat, Kenya imesema inauona mpango wa Morocco kuwa suluhisho pekee la kuaminika na la kweli na njia pekee endelevu.

Kenya, baada ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi mbili na Morocco, pia ilifungua ubalozi huko Rabat siku ya Jumatatu.

Biashara ya pande mbili

Morocco, nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa fosfeti na mbolea, imekubali kuharakisha mara moja usafirishaji wa virutubisho vya udongo nchini Kenya, huku nchi hizo mbili zikipanga kushirikiana katika nishati mbadala, utalii, uvuvi, usalama na masuala ya kitamaduni na kidini, ilisema taarifa hiyo ya pamoja.

Waziri wa mambo ya nje wa Morocco Nasser Bourita aliwaambia waandishi wa habari kuwa msimamo wa Kenya kuhusu Sahara Magharibi, ambao aliuita “sababu ya kitaifa”, ulisaidia kuongeza msukumo mpya katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Kenya inatazamia kusafirisha chai zaidi, kahawa na mazao mapya nchini Morocco ili kusawazisha biashara yake, waziri wa mambo ya nje wa Kenya Musalia Mudavadi alisema kwenye akaunti yake ya X.

Kenya pia iliunga mkono mpango wa Morocco unaozipa mataifa ya Sahel ambayo hayana bahari kupata biashara ya kimataifa kupitia bandari za Atlantic za Morocco, taarifa hiyo ya pamoja ilisema.