Emine Erdogan, ambaye ni mke wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amehutubia jukwaa la kimataifa la familia lililoandaliwa na Wizara ya Familia na Huduma za Kijamii.
Akizungumzia umuhimu wa tukio hilo, Emine Erdogan alisema, “Ni imani yangu kuwa hofu zetu zinafanana. Tuna nia moja kwa sasa, ya kulinda familia zetu dhidi ya vitisho mbalimbali.”
Alionesha matumaini kuwa jukwaa hilo ni “hatua muhimu ya kufikia malengo ya pamoja.”